Sibuka FM

Wananchi wapewa mbinu za kukabiliana na Tembo vamizi.

11 May 2021, 1:24 pm

Wananchi  wilayani  Meatu  Mkoani   Simiyu  wameaswa  kushirikiana   na  wataalamu  wa   Wanyama pori  ili  kudhibiti  Uharibifu unaofanywa na  wanyama  katika  maeneo  yanayozungukwa  na  Hifadhi za  wanyama.

Wito  huo  umetolewa  na  mwakilishi  wa  Mkurugenzi  idara  ya  Wanyama Pori  kutoka  Wizara  ya  Maliasili  na  Utalii   Ndugu  Pellage  Kauzeni  wakati  akihitimisha  mafunzo  ya  Vijana  thelathini  kutoka   wilaya  tatu  za  mkoa  wa  simiyu  zinazopakana  na  Hifadhi  za  Wanyama..

Sauti ya Pellage Kauzeni

        

Kaimu  Mkurugenzi  mkuu wa Taasisi  ya  Utafiti wa  Wanyapori –TAWIRI    Bi Janemary   Ntalwila  amesema  kuwa  vijana  hao  thelathini  wamefundishwa  mbinu  za  kukabiliana  na  wanyama  waharibifu  hasa  wanyama  hao  wanapovamia  kwenye  mashamba  ya  Wananchi.

Sauti ya Janemary Ntalwila

     

Aidha Mkuu  wa  wilaya  ya  Meatu   Ndugu  Joseph  Chilongani  na  mkuu  wa  Wilaya  ya  Bariadi  Ndugu  Festo  Kiswaga   Wakasema  kuwa  Mafunzo  hayo  yamekuja  kwa  wakati  muafaka  kwani  yatajibu  Hitaji  la  wananchi  juu  ya  kupambana  na  wanyama waharibifu  hivyo  Serikali  iwawezeshe  vitendea  kazi..

Sauti ya DC Meatu na DC Bariadi

Kwa  upande  wake  mwenyekiti  wa Chama  cha  mapinduzi  wilaya  ya  Meatu mkoani   Simiyu  Juma  Chazenga   Mwiburi  amesema kuwa  wataalamu  hao  wa  Wanyapori  wamefanya  jambo  zuri  hasa  kuwaelimisha  walengwa  wenyewe  ambao  ni  wananchi  kwani  itasaidia  kudhibiti  tembo  hao  ambao  wamekuwa  wakivamia  mashamba  mara  kwa  mara.

Sauti ya Juma mwiburi  Mw/kiti  ccm  Meatu.

      

Tembo
Wananchi