Sibuka FM

Waziri Mashimba Ndaki akabidhi viti na Meza Shule za Sekondari kwenye Jimbo lake vyenye thamani ya Mil 18..

18 May 2021, 10:30 am

Waziri  wa  Mifugo  na  Uvuvi na  Mbunge  wa  Jimbo  la   Maswa  Magharibi  mkoani  Simiyu  Mh, Mashimba  Ndaki  amekabidhi  Viti  na  Meza  kwa  ajili  ya  wanafunzi  vyenye  thamani  ya  shilingi  Milioni  Kumi  na  nane  ili  kuondoa  Changamoto  ya  Wanafunzi  kukaa  chini.

Mh,  Mashimba  amekabidhi  viti  na  Meza  hivyo  kwa  Shule za  Sekondari   Buchambi, Shishiyu   na  Nyabubinza   kwa  niaba  ya  shule  Kumi  na  nane  za  Jimbo la  Maswa  Magharibi.

Sauti ya Mashimba Ndaki

          

Waziri  Mashimba  pia  ameahidi  kutoa  Komputa  tano  kwa  kila  shule  ya  Sekondari  zilizopo  kwenye  Jimbo  lake  ili  wanafunzi   waendane  na  Uimwengu  wa   Teknolojia..

Sauti ya Mashimba Ndaki
Mashimba Ndaki

             

Awali   akitoa  taarifa  ya  Utengenezaji  wa  Viti  na  Meza   hivyo   kwa  Waziri  wa  Mifugo  na  Uvuvi   na  Mbuge  wa  Jimbo  la  Maswa  Magharibiri  Mh  Mashimba  Ndaki,  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mh, Aswege  Kaminyoge  amesema  kuwa   kwa  sasa  Shule  za  Sekondari  Jimbo  la  Maswa  Magharibi   hazina  upungufu  mkubwa  wa  Madawati..

Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge

               

Kwa  upande  wa  Wananchi wa Jimbo la  Maswa  Magharibi  wamemshukuru   Mbuge  wao kwa  Msaada  alioutoa  wa  viti  na  Meza  kwa  ajili  ya  wanafunzi…

Baadhi ya Wananchi wakishukuru

            

Aidha Sibuka  Fm  imezungumza  na  wanafunzi  ambao  ndio  walengwa  katika  msaada  huo  uliotolewa  na  Mbuge   na  kusema  kuwa  utasaidia  kuongeza  Ufulu  kwa  hapo  awali  walikuwa  wakikaa chini.

Wanafunzi wakimshukuru Mbunge wao.