Uvinza Fm

Wafanyabiashara walia na ulinzi

18/05/2021, 7:33 pm

Na,Mwanaid Suleiman

Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Uvinza Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma wamesema wanashindwa kuongeza bidhaa katika maduka yao kutokana na kuhofia usalama uliopo katika eneo hilo

Hayo yamebainishwa na JUMA RASHID pamoja na TAMIM JACKSON wakati Redio Uvinza fm  ilipofika kutazama namna wafayabiashara wanavyofanyakazi , huku wakisema inawawia vigumu kuongeza bidhaa kutokana nakutokuwepo kwa walinzi wa kutosha

Sauti za Wafanyabiashara

Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara hao bw. JONATHAN  MANYAGA  amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo  na amesema  kwamba atawaitisha wafanyabiashara wote ili kuwapa elimu yakujua umuhimu wa uwepo wa walinzi katika Soko hilo

Sauti ya mwenyekiti wa soko

Naye mwenyekiti wa kijiji cha uvinza  amesema kuwa wanafanya mikakati ya kuweka ulinzi shirikishi ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo mizuri ya ulinzi ili kuepuka vitendo vya kiuhalifu

Sauti ya mwenyekiti wa Kijiji

Aidha kuwepo kwa walinzi katika eneo lolote lile nimoja ya njia zakuwahakikishia Raia ulinzi na usalama wa mali zao.